Mhe. Balozi alikutana na Mkuu wa Idara ya Usafirishaji wa Dawa wa Kampuni ya Serikali ya SAIDAL, Dr. Lydia Azem ambaye alifika Ubalozini. Bi. Lydia alimueleza Mhe. Balozi kuwa mbali na Uzalishaji wa Chanjo, Dawa za Kansa, SAIDAL inatarajia Kuzalisha Insulin za Wagonjwa wa Kisukari mwezi Machi, 2023. Kwa sasa Kampuni hiyo ina Viwanda Vinane (8) na Vituo vitatu vya Usambazaji. Aidha, Kampuni ya SAIDAL inatarajia kusajili TMDA Dawa zake hivi karibuni ili ziweze Kuingia katika Soko la Tanzania.
Mheshimiwa Balozi amempongeza Bi Lydia kwa hatua waliofikia SAIDAL kwenye Uzalishaji na vile vile kwa Kufanya Uamuzi sahihi wa Kusajili Dawa zao Tanzania. Hatua hiyo itaisadia Serikali na Wananchi kwa ujumla kuwa na Vyanzo vingi vya Dawa za Uhakika na kwa Bei ya Ushindani.

