Mhe. Balozi Mej Jen. (Mst) Jacob Gideon Kingu alikutana na Kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi wa Mashirikiano na Mahusiano ya Vyuo VIKUU (Director of Cooperation and Universty Exchanges) wa Wizara ya Elimu ya Juu na Tafiti za Sayansi nchini Algeria Prof. Taher Sahroui. Viongozi hao walizungumzia Mashirikiano ya Sekta ya Elimu ya Juu yaliyopo baina ya Tanzania na Algeria. Kadhalika, Kuongeza wigo kwenye Mashirikiano hayo na Kuanzisha Mashirikiano Pacha biana ya Vyuo Vikuu vya Nchi zote mbili ambayo yatajikita kwenye Ushirikiano wa Tafiti za Sayansi zitakazojumuisha Ziara za Wanafunzi na Wahadhiri.
Kupitia Mashirikiano hayo, Wanafunzi wa Elimu ya Juu wa kada za Sayansi kutoka Tanzania watapata Fursa ya Kusimamiwa Tafiti zao na Wahadhiri/Wataalamu kutoka Tanzania au Algeria na vile vile watakuwa na fursa ya Kushirikiana na wenzao wa Algeria kwenye tafiti zao mbalimbali kama vile za Afya, Uhandisi, TEHAMA, Maji, Jiolojia na Kilimo jambo ambalo litawajengea uwezo zaidi katika Taaluma zao.

