Mhe. Balozi Mej Jen. (Mst) Jacob Gideon Kingu alifanya Mazungumzo na Dr. Moussa Sissoko, Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Afrika waliopo nchini Algeria (CARREFOUR CADENKOSO) katika Ofisi za Ubalozi Jijini Algiers. Katika kikao hicho, Dr. Sissoko alieleza kuwa Jukwaa la “Carrefour Cadenkoso” lipo kwa ajili ya Kuwasaidia Wanafunzi wa Kiafrika wanaofanya Masomo yao nchini Algeria na wale ambao wamemaliza na Kurudi nyumbani kwa kuwapatia Semina za Mafunzo ya Ujasiri Amali, Kuwasimamia katika Uvumbuzi na Kuanzisha Kampuni Changa “Starts-up” ili waweze kuepukana na Utegemezi wa Ajira.
Jukwaa la “Carrefour Cadenkoso” linawakaribisha Wanafunzi wa Kitanzania waliopo nchini Algeria na wale waliohitimu Masomo yao kujiunga na Jukwaa hilo ili kufaidika na fursa mbali mbali za Kiuchumi zilizopo nchini Algeria na Tanzania.
