Mheshimiwa Balozi Mej Jen. (Mst) Jacob Gideon Kingu alikutana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania (TFF) Bw. Wallace J. Karia katika Ofisi za Ubalozi Jijini Algiers. Bw. Wallace alikuwepo nchini Algeria Kikazi kwa ajili ya Kushiriki Ufunguzi wa Kombe la Afrika la Wachezaji wa Ndani (CHAN) ambalo linafanyika nchini Algeria mwaka huu wa 2023.
Mhe. Balozi kwa upande wake amemshukuru Rais wa TFF kwa kutembelea Ubalozi. Aidha, alimshauri Rais wa TFF kuanzisha Makubaliano ya Ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Algeria ili Kubadilishana Uzoefu kwenye Mafunzo ikizingatiwa kuwa Algeria imekuwa ikifanya vizuri katika Mchezo wa Mpira wa Miguu.
