Wahitimu hao wa fani za Afya  (udaktari, ufamasia na udaktari wa wanyama) walifika Ubalozini kwa ajili ya Kuaga rasmi. Aidha wameushukuru Ubalozi kwa Ushirikiano wa karibu na kwa Kutatua changamoto zao kwa wakati kwa kipindi chote walichokuwa wanafunzi. Aidha, wametoa Shukurani  za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria kwa  Ufadhili wa Masomo yao na Kueleza kuwa Algeria ni sehemu sahihi kwa fani za Afya.  Kwa mwaka huu masomo 2021/2022 jumla ya Watanzania 13 wamehitimu Masomo yao ya Elimu ya Juu (shahada ya kwanza na ya pili) katika Vyuo mbalimbali nchini Algeria. 

kwa upande wake Mhe. Balozi Mej Jen (Mst) Jacob Gideon Kingu amewapongeza Wahitimu hao kwa Kumaliza salama Masomo yao na Kuwatakia safari njema. Aidha, Mhe. Balozi aliwasisitiza kuwa Wazalendo na kuzitumia Taaluma zao kwa weledi.