Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ageria Mhe. Iman Salum Njalikai alitembelea viwanda vya karatasi na madaftari vya kampuni ya Hilal vilivyopo jijini Algiers tarehe 22 Septemba 2025.

Ziara hiyo ni muendelezo wa mazungumzo ya Mhe. Balozi na uongozi wa Kampuni ya Hilal yaliyofanyika tarehe 16 Septemba 2025 katika Ofisi za Ubalozi jijini Algiers kuhusu kuimarisha ushirikiano wa biashara kati ya Algeria na Tanzania kupitia fursa ya zilipo kupitia makubaliano ya AfcFTA ambayo Tanzania na Algeria ni wananchama.

Katika ziara yake, Mhe. Balozi alipokelewa na Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje Bw. Chergui Djemoi pamoja na uongozi wa Kampuni hiyo na kutemebelea uniti mbalimbali za uzalishaji na eneo la kuhifadhia bidhaa.

Kwa upande wake Mhe. Balozi aliupongeza uongozi wa Kampuni ya Sarl Hilal kwa uzalishaji wa bidhaa bora na matumizi ya teknolojia na mitambo ya kisasa. Sambamba na hilo Mhe. ameishauri kampuni ya  Hilal kuzitambulisha bidhaa zao kwenye bodi ya viwango Tanzania kwa ajili ya taratibu za kibishara.

Aidha, amewahakikishi kuwa hana mashaka na ubora wa bidhaa zao na Ubalozi utaendelea kuwatambulisha kwa wadau husika nchini ili kuona namna bora ya kufanya nao kazi kwa pamoja.

Kampuni ya Hilal ni moja ya waanzilishi wa viwanda vya uzalishaji wa madaftari, Note book, karatasi za A4 ambao wana hisa ya soko la ndani kwa zaidi ya 40%. Viwanda vingine vikizalisha 60% ya mahitaji ya nchi. Kutokana na Soko la ndani kujitosheleza Kampuni ya Sarl Hilal imelenga kuongeza uzalishaji kawa ajili ya soko la nje ikiwemo Tanzania.