Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Jacob G. Kingu amefanya Ziara ya Kuwatembelea Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Elimu ya Sekondari na Diploma katika Taasisi za Elimu zilizopo Mkoani Ghardaia nchini Algeria tarehe 6 Disemba, 2020.
Mheshimiwa Balozi amewasisitiza Wanafunzi hao Kusoma kwa Bidii na Kuiwakilisha vyema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vile vile, Mheshimiwa Balozi amewashukuru Wakurugenzi wa Taasisi hizo kwa Ufadhili wa Masomo wanaoutoa kwa Vijana wa Kitanzania.
Mheshimiwa Balozi pia ameziomba Taasisi hizo Kuanzisha Mpango wa Kufundisha Lugha ya Kiswahili ili kuwa sehemu ya Mkakati wa Kuelekea kwenye Mashirikiano ya Kiuchumi na Kibiashara.



