Mheshimiwa Balozi, Maj Gen. Jacob G. Kingu amemtembelea Waziri wa Elimu ya Juu na Tafiti za Sayansi wa Algeria Mheshimiwa Abdelbaki BENZIANE Wizarani Mjini Algiers.

Katika Mkutano huo, Viongozi huo walizungumzia  Suala la Kuendeleza Ushirikiano uliyopo katika Sekta ya Elimu ya Juu baina ya Tanzania na Algeria, pamoja na Kuanzisha Mashirikiano  katika Eneo la Tafiti za Sayansi, Mashirikiano baina ya Vyuo Vikuu vya Nchi mbili, pamoja na Kutoa Fursa kwa Lugha ya Kiswahili kuweza Kufundishwa katika Baadhi ya Vyuo Vikuu vya Algeria.