Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, tarehe 09 Oktoba 2025, uliandaa mkutano wa kila mwezi wa nchi wanachama wa SADC zenye uwakilishi nchini Algeria.

 

Mkutano huo, umeendelea kuwa jukwaa muhimu kwa kundi hilo kupata fursa ya kukutana na kujadili masuala mbalimbali ya namna ya kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kiuchumi.