Mheshimiwa Balozi amekutana na Kufanya Mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Taifa la Wamiliki wa Hoteli nchini Algeria Bwana Ahmad OuldBachir. Mheshimiwa Balozi amemueleza Rais wa Shirikisho juu ya umuhimu wa kuwa na Mashirikiano na Tanzania katika kukuza utalii wa Nchi zote mbili. 

Aidha, Mheshimiwa Balozi amemuelezea Rais Fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Utalii kama vile Ujenzi wa Hoteli na Migahawa na Kumhakikishia kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itawapa Mashirikiano Wawekezaji kutoka nchini Algeria ili kufanikisha Azma ya Uwekezaji.

 Rais wa Shirikisho nae ameahidi kuandaa Ujumbe wa Shirikisho la kwenda Tanzania kwa ajili ya Kuona fursa za Uwekezaji zilizopo na Pia amemuomba Mheshimiwa Balozi Kutembelea Vivutio vya Utalii wa Algeria pamoja na Kutembelea Hoteli zao.