Mheshimiwa Balozi amekutana na Rais na Mkurugenzi Mkuuu wa Shirika la Mafuta la Serikali nchini Algeria, Mheshimiwa Toufik HAKKAR katika Ofisi za SONATRACH mjini Algiers.
Mheshimiwa Toufik amemueleza Mheshimiwa Balozi kuwa Shirika la Mafuta la SONATRACH limejikita zaidi katika Kufanya Tafiti za Utafutaji Mafuta na Uchimbaji, kwa Bara la Afrika ndio Shirika la kwanza katika Uchimbaji wa Mafuta.
Kutokana na Uzoefu waliokuwa nao kwenye Mafuta wako Tayari Kushirikiana na Tanzania na Kubadilishana Uzoefu kwa Maslahi ya Pande zote mbili. Kwa upande wake Mheshimiwa Balozi ameomba Kuimarisha Mashirikiano kati ya Shirika hilo na TPDC ya Tanzania hasa katika Maeneo ya Mafunzo na Mazoezi ya Vitendo.
23 Disemba, 2020

