Katika Kuendeleza Mashirikiano na Algeria, Mheshimiwa Balozi Mej Gen. Jacob G. Kingu amekutana na Kufanya Mazungumzo na Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Algeria Mheshimiwa Chakib Rachid Kaid.

Viongozi huo wamezungumzia  Masuala Muhimu ya Mashirikiano ikiwemo Kuimarisha na Kukuza Diplomasia ya Uchumi kati ya Algeria na Tanzania pamoja na Kufanyika kwa Ziara za Kikazi za Viongozi wa Juu wa Nchi mbili kwa lengo la Kusukuma mbele Mashirikiano yaliyopo.