Mhe. Balozi Maj Jen (Mst) Jacob Gideon Kingu alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu Algeria Mhe. Amar Belani leo tarehe 08 Novemba, 2022 katika Wizara ya Mambo Nje. Mhe. Balozi ameipongeza Serikali ya Algeria na Watu wake kwa Kuadhimisha Miaka 68 ya Mapinduzi Matukufu pamoja na Kufanikisha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu uliofanyika Jijini Algiers tarehe 1 hadi 2 Novemba 2022.
Aidha, Mhe. Balozi alieleza Mchango mkubwa wa Algeria katika Bara la Afrika Kuanzia Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika hadi sasa. Viongozi wote wawili walizungumzia Mashirikiano ya pande mbili ikiwemo Kuimarisha Ziara za Viongozi wa juu na Kuendelea Kushauriana Kisiasa baina ya Nchi mbili. Kadhalika, Kuendeleza Mshikamano katika mustawa wa Bara la Afrika hususan katika kukabiliana na changamoto za Uslama na Maendeleo Endelevu.

