Mnamo tarehe 18 Januari, Mheshimiwa Balozi alikutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Shirika la Gesi na Umeme la Algeria SONELGAZ, Bw. Mourad Adjal. Katika Mkutano huo, Viongozi wote wawili walizungumzia Mwendelezo wa Mpango wa Mashirikiano ya Nishati kwenye Suala la Umeme na Gesi kati ya SONELGAZ, TPDC na TANESCO. AmbapoTimu ya Wataalamu kutoka pande zote mbili inatarajia kuwa na Vikao vya Zoom kwa ajili ya Maandalizi ya Kukutana na Kukamilisha Mchakatao wa Makubaliano ya MoU.

