Mheshimiwa Balozi amekutana na Kufanya Mazungumzo na Wanadiaspora wanaoishi nchini Algeria. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Balozi amewaeleza Wanadiaspora namna Tanzani invyopiga hatua Kimaendeleo, huduma za Jamii zimeboreshwa zaidi na Miradi Mikubwa ya Ujenzi wa Miundo mbinu imeweza kutekelezwa ikiwemo Ujenzi wa Barabara, Standard Guage Railway na Viwanja vya Ndege. 

Hivyo amewataka Wanadiaspora Kuitangaza Tanzania kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara kwenda Kuwekeza na Kufanyabiashara na Tanzania na Watapokelewa Vizuri. Mheshimiwa Balozi pia amewasihi Wanadiaspora Kutumia Kipato chao kuwekeza nchini Tanzania kwani kutasaidia sana kukuza Uchumi wa Taifa.