Mhe. Balozi Mej Jen (Mst) Jacob Gideon Kingu alikutana na Kufanya Mazungumzo na Waziri wa Utalii na Sanaa wa Algeria Mhe. Yacine Hamad katika Ofisi za Wizara ya Utalii na Sanaa Jijini Algiers. Kupitia Kikao hicho, Viongozi wote wawili walizungumzia Umuhimu wa Kuendelea Kushikamana kwa Nchi mbili kwenye Sekta ya Utalii. Hatua hiyo ni pamoja na Kuvitangaza vivutio vya Utalii vya pande zote mbili na Kuwahamisha Wananchi Kutembeleana na Kushiriki katika Makongamano ya Kimataifa ya Utalii yanayoandaliwa katika nchi hizi.
Aidha, Viongozi hao walizungumzia suala la kuwepo usafiri wa moja kwa moja ili kuwawezesha Watalii na Wafanyabiashara kusafiri kwa urahisi na gharama nafuu. Waziri wa Utalii na Sanaa Mhe. Yacine Hamad amelipokea Ombi hilo na Kuahidi Kulifanyia Kazi.


