Mheshimiwa Balozi, Maj Gen. Jacob G. Kingu, mnamo tarehe 22 Disemba, 2020 amekutana na Meneja Mkuu wa "Chamber of Commerce and Industry" nchini Algeria Bibi Ouahiba Behloul.

Viongozi hao wamejadili Mikakati ya Kukuza Mashirikiano ya Kibiashara na Viwanda kati ya "Chamber of Commerce and Industry" ya Algeria na "Chamber of Commerce, Industry and Agriculture" ya Tanzania.

Mheshimiwa Balozi pia amemuelezea Meneja Mkuu kuhusu Fursa za Biashara zilizopo baina ya Nchi mbili na Kumuelezea Taratibu za Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania  pamoja na Kumkabidhi Mwongozo wa TCCIA na TIC.