Katika muendelezo wa ushiriki wa Tanzania kwenye IATF2025, Mhe. Balozi Iman Njalikai pamoja na Ujumbe wa PURA walipata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mafuta la Serikali (Sonatrach) Bw Rachid  Hachichi katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Algiers tarehe 07 Sept 2025.

 

Kwa upande wake Mhe. Balozi alitoa shukran zake za dhati kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Sonatrach na TPDC akigusia ziara mbalimbali za Taasisi za nishati nchi ambazo zimekuja nchini Algeria kwa ajili ya kupata uzoefu na biashara kama vile ujumbe wa TFC, ujumbe wa TPDC na Ujumbe wa REA.

 

Kwa pamoja Viongozi wote wawili walijadili maeneo ya ushirikiano na kulipa kipao suala zima la mafunzo na ushirikiano katika utafiti wa mafuta na gesi.

 

Sonatrach ni moja kati ya Kampuni bora duniani kwenye eneo la mafuta na gesi. Kupitia rasimu zilizopo za ushirikiano wako tayari kupokea mahitaji ya Tanzania katika kuwajengea uwezo wa Rasilimali watu.