Tarehe 25 Machi 2025, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ujumbe wake aliwasili nchini Algeria kwa lengo la kuwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenda kwa Mhe. Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria.
Mheshimiwa Rais Mstaafu alipata fursa ya kukutana, kufanya Mazungumzo na kuwasilisha ujumbe huo kwa Mheshimiwa Rais Tebboune Tarehe 25 Machi 2025. Ziara hiyo, ilikuwa ni sehemu muhimu katika kuimarisha uhusiano mzuri, wa muda mrefu na wa kihistoria ulioasisiwa na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania na Hayati Ahmed Benbella, Rais wa kwanza Algeria.
Akiwa nchini Algeria, Mhe. Rais Mstaafu pia alipata fursa ya kutembelea Ofisi za Ubalozi pamoja na kupata taarifa za shughuli mbalimbali za Ubalozi kutoka kwa Mhe. Balozi Njalikai, Balozi wa Tanzania nchini Algeria.




