Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Jacob G. Kingu amemtembelea Rais wa Kamati za Olimpic Barani Afrika (ACNOA) Mheshimiwa Moustapha Berraf katika Ofisi yake iliyopo Mjini Algiers. Katika Mazungumzo yao Mheshimiwa Berraf amesisitiza kwa Tanzania  inahitaji kuekeza kwenye Michezo kwa vijana  kuanzia Miaka 10 ili kuweza kupata Wanamichezo Bora siku za usoni. 

Aidha, Bwana Berraf ameahidi Kutembelea Tanzania na Kuisaidia Tanzania katika Maeneo mbali mbali ya Michezo kama vile Mafunzo ya Madaktari wa Michezo, Makocha Mafunzo ya Utawala.