Katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata fursa za Mafunzo ya Elimu ya Juu nchini Algeria katika Fani za Kimkakati, Mheshimiwa Balozi amezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika Wizara ya mambo ya nje, Mheshimiwa Balozi Isaad MAANDI kuhusu kuiongezea Tanzania Nafasi za Ufadhali wa Masomo ya Elimu ya Juu kwa Fani za Uhandisi, Afya na Nishati pamoja na Mpango wa Kufundisha Lugha ya Kiswahili Vyuo Vikuu nchini Algeria. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Afrika ameeleza kuwa Algeria ipo tayari Kuipatia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nafasi itakazoona inafaa ili kujenga uwezo wa watu wake.