Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Pindi H. Chana akiambatana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Sanaa, Mh. Tabia M. Maulid walipata fursa ya Kukutana na Mwenyeji wao Waziri wa Vijana na Michezo wa Serikali ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Abderrahmane Hammad katika Afisi za Wizara ya Michezo Jijini Algiers tarehe 03 Juni, 2023.

Kupitia Kikao hicho, Viongozi hao walikubaliana Kuendeleza Diplomasia ya Michezo kati ya Nchi mbili na Kuanzisha Kikosi Kazi kitakachojumuisha Wataalamu kutoka Algeria, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kuja na Mapendekezo ya Maeneo Muhimu ya Ushirikiano kwa ajili ya Ustawi wa Sekta ya Michezo na Vijana.

Sambamba na hilo, Mhe. Waziri Pindi. H. Chana amemualika Waziri Abderrahmane Hammad Kutembelea Tanzania ikiwa ni Sehemu ya Kuimarisha Ushirikiano kati ya nchi mbili hizi.