Ubalozi umeendelea Kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa Kukutana na Kufanya Mazungumzo na Kampuni ya Kimataifa ya Uzalishaji wa Dawa  za Binadamu ya HIKMA katika Afisi zao  Jijini Algiers, tarehe 04/04/2023. HIKMA ni kati ya Kampuni  zinazoongoza kwenye Uzalishaji wa Dawa za Binadamu nchini Algeria na ni ya pili kwa Uzalishaji wa Dawa za Generics. Kupitia Mkutano wa huo, Kampuni ya HIKMA imeeleza kuwa tayari imeshapata Mwongozo wa Usajili wa Dawa kutoka TMDA pamoja na Taarifa za Soko kupitia MSD na inaendelea  Kufanya Stadi ya Soko la Dawa zao kwa ajili ya Biashara na Uwekezaji.

Pamoja na Mkutano huo, Ubalozi  pia ulipata fursa ya Kutembelea moja ya Kiwanda chao cha Uzalishaji wa Dawa aina ya Peniciline ambazo ziko kwenye mfumo wa unga (powder) kilichopo jijini Algiers.