Mheshimiwa Balozi na kushoto mwake ni Mhandisi Abdelmalik kutoka Kampuni ya AMENHYD, akitembelea mradi wa Maji Taka wenye ukubwa wa ekari 22 uliopo kando ya Jiji la Algiers. Dampo hilo limegeuzwa kuwa Bustani na Kuwekewa Mitambo ya Kuzalisha Biogas MW.3 pamoja na Kuchakata Maji Taka yailiyofunikwa na udongo na Kuzalisha maji safi kama inavyooneka kwenye picha hapo chini.

     Kampuni ya AMEN HYD tayari imefanya Mazungumzo ya Awali na Wizara ya Maji ya Tanzania Bara na Visiwani kwa Lengo la Kuwekeza na Kuhamisha Maarifa ya Kuchakata Maji, Maji Taka, Kutunza Mazingira pamoja Kuzalisha Nishati Mbadala.