Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliungana na  Wazazi katika Mahafali ya Wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Udaktari iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa CIC jijini Algiers tarehe 21/01/2023. Mahafali hiyo ilijumuisha Wahitimu wapatao 1800 kutoka Chuo Kikuu cha Algiers -1 wakiwemo Watanzania wawili (2) Dk. Mohamed Abdelaziz pamoja na Dk. Raymond Albert Mwaituka.