Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekuwa mstari wa Mbele katika kuhakikisha kuwa Bidhaa za Kilimo za Tanzania zinapata Soko nchini Algeria. katika kuzitangaza Bidhaa hizo Ubalozi umeshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Kahawa ya Siku nne yaliyofanyika Mjini Algiers. 

Katika Maonesho hayo, Wafanyabiashara wa mazao mbali mbali walitembelea Banda la Ubalozi na Kuona Sampuli za Bidhaa kama vile Kahawa, Korosho, Karafuu, Mchele, Maharage, Pilipilimanga na Kupatiwa Mwongozo wa Kufanyabiashara na Tanzania.

Mwitikio wa Algeria kuhusu bidhaa za Tanzania ni Mkubwa na Ubalozi unatoa Wito kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kutembelea nchini Algeria ili kuweza kufanya mazungumzo ya Kibiashara na Wenzao wa Algeria hasa kwa Kushiriki katika Maonesho  na Kuonesha Bidhaa zao.