Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria umelipa Kipaumbele suala la kutangaza Utalii wetu nchini Algeria. Katika kufanikisha Malengo hayo, Ubalozi chini ya Mheshimiwa Balozi Omar Omar Yussuf Mzee umeshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii yaliyofanyika kwa siku nne Mkoani Oran.

Ushiriki wa Ubalozi ulikuwa na tija kubwa kwani Viongozi mbali mbali wa Serikali walitembelea Banda hilo akiwemo Waziri wa Utalii, Waheshimiwa Balozi, Mawakala wapatao mia mbili (200), Waandishi wa Habari pamoja na Wadau mbali mbali wa Utalii ambao wote walipatiwa Mwongozo wa utalii wa Tanzania pamoja na Vivutio vya Kutembelea kama vile Zanzibar, Mlima Kilimanjaro na Serengeti. Na Mwongozo wa Upatikanaji Viza.