Ubalozi ulifanya Mazungumzo na Dkt.  Amine Bensemmane Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Masuala ya Kilimo GRFI katika Ofisi za Ubalozi jijini Algiers. Dkt. Bensemmane  ambaye pia ni Mratibu na Msimamizi Mkuu wa Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo nchini Algeria maarufu kama SIPSA alieleza kuwa Maonesho ya mwaka huu yatakuwa  ni Toleo la 21 na yatafanyika Jijini Algiers kuanzia tarehe 22 hadi 25 Mei, 2023.

Maonesho hayo yamelenga kuwa na Taaswira pana zaidi kwa Kuzishirikisha ipasavyo Nchi za Afrika ili kuwa na Usalama wa Chakula ambapo Mgeni rasmi itakuwa ni nchi ya Senegal. Maonesho yatajikita kwenye Kilimo cha Kisasa, Uzalishaji, Uchakataji wa Mazao ya Kilimo, Usafirishaji na Utunzaji. Aidha, Maonesho yatakuwa na fursa za Mikutano ya B2B kwa Kampuni zitakazoshiriki.

Ubalozi unatoa wito kwa Kampuni za  Kilimo za Tanzania Kutembelea na Kushiriki katika Maonesho hayo ili Kukutana na Wataalamu wa Kilimo kwa ajili ya Kubadilishana Uzoefu na Kutafuta Soko la Mazao ya Kilimo.

Pichani Mhe. Balozi akiwa na Dkt. Bensemmane na Bw. Brahim  Zitouni Mtaalamu wa Uchumi kwenye Kilimo.