Ubalozi ukifanya Wasilisho la Fursa za Uwekezaji nchini Tanzania kwenye Kikao cha B2B na Wawekezaji na Wakandarasi wa Ujenzi. Pichani kulia mwa Mhe. Balozi ni Waziri wa Biashara Mstaafu wa Algeria, Mhe. Said Djellab na Kushoto kwake ni Mhandisi Luteni Kanali Juma Muhsini Mvumbo, Meneja wa SUMA JKT Ujenzi, Kanda ya Nyanda za Juu.
Timu ya Ubalozi na Wawekezaji wa Sekta ya Ujenzi baada ya Kikao cha ‘B2B’ pembezoni mwa Maonesho hayo. Kupitia Kikao hicho, Ubalozi ulifanya Mazungumzo na Kampuni kubwa za Uzalishaji wa Vifaa muhimu vya Ujenzi kama vile vifaa vya Umeme, Nondo, Saruji, Aluminium na PVC kwa ajili ya kuwekeza na Kuingia Ubia na Watanzania ili Kuhamisha Maarifa ya Teknolojia ya Ujenzi wa Kisasa nchini Tanzania.


