Timu ya Ubalozi iliwatembelea Wanadiaspora na Wanafunzi wanaosomo katika Taasisi mbali katika Mkoa wa Ghardaia. Ziara hiyo ni katika Utekelezaji wa Mpango wa Ubalozi wa kuwahakiki na Kuwatambua Watanzania waliopo nchini Algeria pamoja na Kufahamu Maendeleo na Shughuli wanazozifanya. Kupitia Ziara hii, Ubalozi uliwatembelea Wanafunzi wa Taasisi ya Maahad Al-hayat na Taasisi ya Ami Said ambao wanasomea Masomo Sekondari na Vyuo. Aidha, Ubalozi ulikutana na wanadiaspora na familia zao na Kuwaeleza fursa za Kiuchumi wanazoeza Kufaidika nazo wakiwa nchini Algeria. kwa sasa Mkoa wa Ghardaia una watanzania wapatao 38. idadi hiyo hiyo inajumuisha Wanafunzi na Wanadiaspora na familia zao.


