Ubalozi ulishiriki katika Ufunguzi wa Kongamano la Biashara la AFRIKA BUSINESS FORUM lililofanyika tarehe 5 hadi 7 Machi, 2023. Ushiriki huo ni mpango wa Ubalozi wa Kuendeleza Kutangaza Diplomasia ya Uchumi kupitia Majukwaa mbali mbali kwa lengo la Kutangaza fursa za Biashara na Uwekezaji na Kuwavutia Wawekezaji wa Nje Kuekeza nchini Nchini Tanzania.
Kongamano hilo la Biashara lilishirikisha Balozi ya zaidi ya 22 za Afrika, kadhalika Kampuni za ndani na Nje ya Algeria ambazo zilionesha Bidhaa zao na Kupata fursa ya kuwa na Vikao vya B2B.
Majukwaa ya namna hii yanaonesha utayari wa Algeria wa Kujenga Ushirikiano wa Kiuchumi na Ndugu zake wa Afrika. Hivyo, ni vyema Wafanyabiashara wa Tanzania wakaliangalia Soko la Kibiashara la Nchi hii ya Afrika ya Kaskazini kwa lengo la Kuchangamana nao ili kukuza Uchumi kati ya nchi hizi mbili.
Pichani Mhe. Balozi akiwa katika Vikao vya B2B pamoja na Kutembelea Mabanda ya Wafanyabiashara walioshiriki katika Kongamano hilo


