Ubalozi ulipokea Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Kitanzania kutoka Kampuni ya ATN Petroleum ya Tanzania Bw. Abdelatif T. Nahdi na Bw. Mohammed Khelef Mohammed Shein ambao walifika Ubalozini kwa ajili ya Kuunganishwa na Wafanyabiashara na Wawekezaji Nchini Algeria.
Ubalozi uliuwanganisha Wafanyabiashara hao na Viwanda vya Uzalishaji wa Dawa za Binadamu, Kiwanda cha Sophal kilichopo Oran na Kiwanda cha Biopharm kilichopo Algiers. Kadhalika, walipata fursa ya Kuunganishwa na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Sekta ya Ujenzi, Mafuta naUtalii.







