Wanafunzi wapya wa Tanzania waliowasili nchini Algeria kwa ajili ya Mhula wa Masomo wa 2024\2025 wameaswa kutumia vema fursa hiyo adhimu kwa kufanya juhudi katika masomo na kuzingatia taratibu na sheria za nchi wenyeji wakati wote wa masomo yao.
Hayo, yalisemwa leo Tarehe 27 Oktoba 2024 na Mhe. Balozi Njalikai wakati akiwakaribisha wanafunzi hao wa Kitanzania waliochaguliwa kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Algeria kwenye Ofisi za Ubalozi jijini Algiers.


