Mhe. Balozi Maj Gen (Mst) alitembelea Maabara ya Orion Lab ya  Kuzalisha dawa za Kutibu Ugonjwa wa  Kansa iliyopo Mkoani Oran. Awali Mheshimiwa Balozi alitembelea Maabara hiyo mwezi Novemba, 2021 ikiwa katika hali ya Ujenzi. Katika Ziara yake hii, Mhe. Balozi alikutana na Mmiliki wa Maabara hiyo Bwana  Seddik AMRY na Kutembelea Vitengo mbali mbali vya Uzalishaji. Maabara hiyo imekamilika kwa Asilimia 99% na inasubiria Kuzinduliwa Rasmi mwezi Oktoba, 2022. Orion lab ni katika Maabara chache  nchini Algeria zinazozalisha Dawa za Kutibu Ugonjwa wa Kansa.