Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Jacob G. Kingu akiwa na Mwenyeji wake Bwana Yahia Meziane, wamefanya Ziara ya Kutembelea Kilimo cha Michungwa ya Kisasa (Highbrid) aina ya Thomson katika Mkoa wa Tipaza.

Bwana Yahia, amemueleza Mheshimiwa Balozi kuwa Machungwa aina ya Thomson yanalimwa kwa wingi nchini Algeria na yana Soko kubwa kutokana na Ladha yake na vile vile kuwa hayana mbegu ndani. Mheshimiwa Balozi amemshauri Bwana Yahia Kuuhamisha Utaalamu huo wa Kilimo na kwenda Kuwekeza nchini Tanzania.

19 Disemba, 2020