Ubalozi  umempokea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda ambaye yuko kwenye Ziara ya Kikazi nchini Algeria kwa muda wa siku tano (5) kuanzia tarehe 28 Novemba, 2022.  Katika ziara yake hiyo, Mkuu wa Majeshi  ameambatana na Maafisa wa Ngazi za Juu kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Mkuu wa Majeshi alipokelewa  na Mwenyeji wake, Jenerali Said Chengriha  katika Makao Makuu ya Jeshi. Wakuu hao walieleza Utayari na Utashi wa Kuimarisha Mashirikiano ya Kiulinzi na Kiusalama na Kubadilishana Uzoefu katika Suala zima la Kupambanda na Ugaidi kwa Maslahi ya pande zote mbili na Afrika kwa ujumla.

Aidha, Mkuu wa Majeshi alifika Ubalozini na Kupokelewa na Mhe. Balozi Maj Jen (Mst) Jacob Gideon Kingu pamoja na Maafisa wa Ubalozi ambapo pia alipatiwa Taarifa fupi ya Maendeleo ya Ubalozi na Fursa za Mashirikiano zilizopo hususan kwenye eneo la Diplomasia ya Uchumi ikiwemo eneo la Ulinzi na Usalama. Ubalozi unatarajia Ziara ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania hapa Algeria kuwa ni Mwendelezo Mzuri wa Mashirikiano na itafungua fursa zaidi kwa pande zote mbili..