Mwakilishi na Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wahamiaji "International Organisation for Migration" nchini Algeria, Mheshimiwa Paolo Giuseppe CAPUTO amemtembelea Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Maj Gen. Jacob G. Kingu Ubalozini Mjini Algiers.

Viongozi hao wamezungumzia Mambo mbali mbali ya Mashirikiano ikiwemo Mchango wa IOM katika Kutatua Changamoto zinazowakabili Wahamiaji ikiwa ni pamoja na Kuwasafirisha Wahamiaji waliokwama na Kuwarudisha Katika Nchi zao.

Aidha,  Mheshimiwa CAPUTO  ameahidi  kuwa IOM itaendelea Kushirikiana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wote katika kutatua Changamoto zinazohusu Wahamiaji. 
 

Tarehe 13 Disemba, 2020