Rais wa Kamati za Olimpiki Barani Afrika (ACNOA), Mheshimiwa Mustapha Berraf amemtembelea Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria Mheshimiwa Maj Gen. Jacob G. Kingu Ofisini kwake Mjini Algiers. Ziara hiyo imefanyika tarehe 10 Disemba, 2020.

Aidha, Mheshimiwa Berraf amemwelezea Mheshimiwa Balozi Umuhimu wa Tanzania Kuwaandaa mapema Vijana Wakitanzania Kimichezo ili waweze Kushiriki katika Michezo ya Afrika  (African Games) itakayofanyika 2023 nchini Ghana ambayo itasimamiwa na Kamati za Olimpiki Barani Afrika. Ushiriki na Ufaulu wao katika Michezo ya Afrika utawapatia Nafasi Kubwa Kushiriki na Kushinda Medali katika Mashindano ya Olimpiki.