Algeria ni Mwagizaji Mkuu wa Pili wa Ngano barani Afrika baada ya Egypt. Hata hivyo, Serikali ya Algeria ina mkakati  wa Kupunguza Uagizaji wa Bidhaa hiyo na Badala yake Kuwekeza kwenye Kilimo cha Kisasa katika Mikoa ya Jangwani kama vile  Mkoa wa Menia hususan katika Uzalishaji wa Mbegu ambazo zimekuwa ghali katika Soko la Dunia. Ubalozi umeweza Kufanya Ziara ya Kikazi katika Mkoa huo na Kukutana na Wakulima wa  Kilimo cha Ngano na Mahindi. Mfumo unaotumika ni  wa umwagiliaji kwa njia ya Pivot. Shamba moja (1) linakuwa na ukubwa kati ya ekari 40 hadi 50 na Kisima kimoja chenye urefu wa mita kati ya 250 hadi 300, ekari moja inatoa kati ya Tani 6 hadi 6.5.

Katika Kuungana na Juhudi za Serikali za Kuipa Kipaumbele Sekta ya Kilimo, Wakulima wa Tanzania ni vyema wakajielekeza kwenye Kilimo cha Kisasa na wanaweza Kubadilishana Uzoefu na Wakulima wa Mkoa wa Menia Algeria kwenye mfumo wa Umwagiliaji, Matumizi ya mbolea na Dawa ili kuwa na Kilimo chenye Tija zaidi ambacho kitalisaidia Taifa Kujitosheleza kwa Vyakula na Kuuza Nje.