Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Salum Njalikai leo Disemba, 28, 2023 alifanya mazungumzo na Waziri wa Vijana na Michezo wa Algeria, Mhe. Abderrahamane Hammad katika ofisi za Wizara ya Michezo jijini Algiers. Kwa pamoja wamekubaliana kukamilisha Rasimu ya Ushirikiano wa Sekta ya Michezo ili iweze kusainiwa mwanzoni mwa mwaka 2024 na kuanza utekelezaji wake kwa maslahi ya vijana wa nchi zote mbili. Aidha, pande zote mbili wemekubaliana kuendeleza na kukuza ushirikiano wa sekta ya michezo hususan kubadilishana uzoefu katika ngazi ya wataalamu.