Mhe. Balozi Iman S. Njalikai  leo tarehe 3 Sept 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika   Bw. Khelifi Abdelnour katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje Jijini Algiers.

Viongozi hao wamejadili masuala ya uhusiano wa uwili katika sekta Anga, usafirishaji wa majini na michezo.

Kadhalika Ushirikiano wa kikanda ikiwa ni pamoja na uungwaji mkono katika nafasi mbalimbli za chaguzi za kikanda na kimataifa.