Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman S. Njalikai alifanya mazungumzo na Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu wa Afrika (CAAID), Dkt Amine Boutalbi katika Ofisi za Ubalozi jijini Algiers tarehe 26 Oktoba, 2023.

Kupitia Kikao hicho, Ubalozi na  Kituo cha CAAID umejipanga kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Algeria pamoja na Kushiriki makongamano ya uwekezaji na biashara yanayoandaliwa na Kituo cha CAAID mwezi Mei 2024 na Maonesho ya Sabasaba yanayofanyika nchini Tanzania ili kuona fursa zilizopo kwa kila upande.

Aidha, Kikao kilijadili uwezekano wa kuandaa kongamano maalum la wafanyabishara wa Algeria nchini Tanzania mwaka 2024. Kongamano ambalo litazaa makubaliano ya kibiashara na wafanyabiashara wa Tanzania kupitia fursa zilizopo.