Mheshiwa Iman Njalika Balozi wa Tanzania nchini Algeria, amekutana na kufanya Mazungumzo na Bw. Naserdine Boutera Mratibu Mkuu wa mkutanao wa ARIS (AFRICA REAL ESTATE INOVATION SUMMIT) katika ofisi za Ubalozi jijini Algiers.Wawili hao wamejadili umuhimu wa Tanzania katika ushiriki wa Mkutano huo na kusisitiza Mashirika ya nyumba Kutoka Tanzania kutangaza bidhaa kupitia jukwaa la AFRICA REAL ESTATE INOVATION SUMMIT.