Ubalozi kwa Kushirikiana na Mwakilishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bi. Latifa Abadalla Kigoda ulishiriki katika Kongamano la Uwekezaji na Biashara Afrika (AFIC9) lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu wa Afrika (CAAID) katika hoteli ya Sheraton Jijini Algiers tarehe 16 na 17 Mei, 2023. Kupitia Jukwaa hilo, Ubalozi ulifanikiwa Kutangaza fursa za Uwekezaji na Biashara zilizopo nchini Tanzania. Aidha, Ubalozi ulitumia Jukwaa hilo muhimu, Kuwaalika Wawekazaji na Wafanyabiashara Kutembelea Tanzania na Kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya 47 ya Dar es Salaam (Sabasaba).