Ubalozi ulishiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Algiers ikiwa ni sehemu ya Juhudi za Kutangaza Diplomasia ya Uchumi katika Sekta ya Utalii. Maonesho hayo yalihudhuriwa pia na Mawakala wa Utalii kutoka nchini Tanzania (Jahazi Tour na Palm Tour). Nchi mbali mbali zilizshiriki Maonesho hayo kama vile, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudia Rabia, Cuba,  Mauritania, Uturuki, Tunisia nk. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mhe. Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mhe. Aimen Benabderrahamane ambaye pia alipata fursa ya Kutembelea Banda la Tanzania na Kupatiwa Maelezo Mafupi juu ya Fursa na Vivutio vya Utalii vilivyopo nchini Tanzania. Aidha, Mabalozi kadhaa, kama vile Afrika ya Kusini, Burkina Faso, Niger, Ethiopia, Namibia nk. Walitembelea Banda la Tanzania.