Baada ya Mheshimiwa Balozi  Kufanya Mazungumzo na Bwana Reda Abeid, Mwekezaji kwenye Sekta ya Umeme, Mheshimiwa Balozi alitembelea Kiwanda cha METGAVE katika Mkoa wa Tlemcen. Kiwanda hicho cha Kisasa kinashughulika na Uzalishaji wa Nguzo za Umeme wa kati na Umeme wa chini (medium volt and low volt) na Bidhaa mbali mbali za Chuma pamoja na Galvanic. Mheshimiwa Balozi amewaalika Kampuni ya METGAVE kwenda Kuwekeza nchini Tanzania.

Kampuni ya METGAVE wameeleza kuwa wako tayari kwenda Tanzania kwa ajili ya Uwekezaji na Kuona fursa zilizopo na Mazingira ya Uwekezaji.