Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe January Y. Makamba ambaye yupo kwenye Ziara ya Kikazi nchini Algeria amekutana na Kufanya Mazungumzo na Waziri wa Nishati wa Algeria, Mhe. Mohamed Arkab katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini Jijini Algiers tarehe 17 Oktoba, 2023.

Waziri Makamba alieleza kufurahishwa na hatua ya mwisho iliyofikiwa mwezi Agosti, 2023 ya Kusaini Makubaliano ya Ushirikiano katika ya Algeria na Tanzania kwenye eneo la Nishati kati ya TANESCO na SONELGAZ, TPDC na SONELGAZ pamoja na TPDC na SONATRACH. Ushirikiano ambao unagusa sekta ya umeme, mafuta na gesi. Aidha, Waziri Makamba ameomba utekelezaji wa Makubaliano hayo kuweza kuanza mapema iwezekanavyo na kuhuisha Kikosi Kazi kilichopewa jukumu hilo kifanye kazi.

Kadhalika, Waziri Arkab alieleza utayari wao kama Wizara ambayo pia ni Maelekezo na Vipaumbele vya Serikali ya Algeria Kuimarisha Ushirikiano wa Nishati na Tanzania. Aidha, Waziri Arkab alitilia Mkazo kuwa Kikosi Kazi kitaanza kukutana na Kuandaa mpango Kazi  wa maeneo yote ya makubaliano ndani ya mwezi wa Oktoba, 2023.