Tanzania na Algeria zakubaliana kuimarisha ushirikiano kwenye eneo la utunzaji kumbukumbu na nyaraka muhimu. Makubaliano hayo, yalikuwa sehemu ya Mazungumzo ya tarehe 28 Oktoba, 2024, kati ya Mhe. Balozi Njalikai na Dkt. Mohamed Bounaama, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Utunzaji Kumbukumbu na Nyaraka muhimu za Serikali ya Algeria, katika Makao Mkuu ya Idara hiyo jijini Algiers.
Wawili hao wamekubaliana kuweka kipaumbele katika kubadilishana uzoefu na kuratibu makongamano ya pamoja yenye lengo la kudumisha taswira ya kihistoria, kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili.