Ubalozi uliipokea Timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Star na ile ya Under Twenty ambazo ziliwasili Jijini Algiers tarehe 8 na tarehe 9 kwa ajili Mechi za Kirafiki. Mhe. Balozi Mej. Jen. (Mst) Jacob Kingu aliambatana na Maafisa wa Ubalozi katika Mapokezi hayo . Sambamba na hilo, Mhe. Balozi alikutana na Timu zote mbili, Twiga Star na Tanzanite pamoja na Mkuu wa Msafara kwa kuwakaribisha Nchini Algeria na Kuwatakia Ushindi kwenye Michezo yao mitatu iliyopangwa Kuchezwa tarehe 9 hadi 11 Aprili, 2023. Aidha, Ubalozi uliiungana na Timu hizo kwa Kufika Uwanjani na Kuwapa Hamasa katika Mechi zote Tatu.
Matokeo ya Michezo hiyo, Mchezo wa kwanza Twiga Star ilipoteza mchezo wake dhidi ya Algeria Mabao 4-0, Mechi ya Pili, Tanzanite ilipoteza kwa Kufungwa Bao 1-0 na Mchezo wa Marudiano kati ya Twiga Star na Algeria kadhalika, Twiga Star ilipoteza kwa Kufungwa Mabao 3-0.
Pamoja na Kupoteza Michezo yote mitatu, Vijana waliipeperusha Bendera ya Taifa kwa Kuonesha Mpira mzuri na wa Upinzani kwa Wapinzani wao. Mchezo huo pia ulikuwa ni fursa ya Kuwajengea Uwezo zaidi na Kuona Maeneo yanayohitaji Kusawazishwa ili kuwa na Timu Imara.