Ubalozi ulishiriki katika Ufunguzi wa Maonesho ya Vinywaji ya BEVALG yaliyofanyika jijini Algiers kuanzia tarehe 6 hadi 8 Machi, 2023. Maonesho hayo yalijumuisha Kampuni mbali mbali za Uzalishaji wa Vinywaji Baridi, Maji, Maziwa na bidhaa zitokanazo na Maziwa kama vile mtindi na yogat nk. Aidha, Maonesho pia yalishirikisha Kampuni za  Ndani na Nje za Utengenezaji wa Mitambo ya Kuchakata Mazao ya Kilimo kwa ajili ya Vinywaji na Vifungashio.

Ubalozi umeona fursa iliyopo katika eneo hilo ambalo wafanyabiashara Watanzania wanaweza Kufaidika kwa Kuingia Ubia na Waalgeria katika Kuanzisha Viwanda vidogo na vya kati vya Vinywaji hususan katika uchakataji wa Matunda ili Kuongeza thamani ya Mazao ya Kilimo.

Pichani Mhe. Balozi akizungumza na Wawekezaji wa Algeria kuhusu fursa za Uwekezaji nchini Tanzania wakati akitembelea Mabanda ya Maonesho baada ya Ufunguzi rasmi.